SFH Banner
DVD ITEM

Chini ya mti wa Mupundu

Wahudumu wa kujitolea katika kuwatunza watu majumbani kwao wenye HIV/UKIMWI na Kifua Kikuu katika jimbo la Shaba la Zambia.

Zambia, kama nchi nyingine nyingi katika eneo la Afrika kusini mwa Jagwa, inakabiliwa na kuenea kwa magonjwa mawili yanayoangamiza ya HIV na Kifua Kikuu. Idadi kubwa ya watu walioathiriwa na HIV na Kifua Kikuu wana mahitaji mengi ya haraka: sio tu ya tiba na matunzo, lakini pia mahitaji ya vitu, msaada wa kijamii, kisaikolojia na kiroho.

Filamu au video hii inaonyesha mpango mpya wa matunzo ya wagonjwa majumbani kwao katika miji 23 yenye mapato ya chini katika jimbo la Shaba la Zambia. Ukiwa umerakibishwa na Dayasis ya kikatoliki ya Ndola, mpango huu umeunganisha udhibiti wa Kifua Kikuu katika matunzo ya nyumbani kwa watu wenye HIV/UKIMWI na familia zao.

Ufunguo wa mafanikio ya mpango huu katika jimbo la Shaba ni jukumu lililochukuliwa kutekelezwa na wahudumu wa kujitolea zaidi ya 500 – wengi wao ni wanawake – ambao wanasaidiwa na wauguzi wa jamii na kusaidiwa kwa huduma zinazotolewa na hospitali. Filamu au Video hii inaonyesha mahojiano mengi ya wahudumu wa kujitolea na familia wanazozitembelea nyumbani. Inaonyesha jinsi udhibiti wa Kifua Kikuu na matunzo ya nyumbani kwa watu wenye HIV/UKIMWI vinavyoweza kujiimarisha na kuwa na uzito mkubwa.

FB Productions na Strategies for Hope.

 

2000; dakika 35; muziki Distro Kuombokop, Zambia.