SFH Banner
DVD ITEM

Naweza Kufanya Nini?

Maelezo kuhusu Virusi vinavyo sababisha UKIMWI na Ujumbe wa Gideon Byamugisha.

Gideon Byamugisha ni mchungaji aliyebarikiwa katika kanisa la Anglikana na Kasisi Kiongozi wa Kanisa la Mt. Paulo, Dayosisi ya Namirembe, Uganda. Anafanya kazi World Vision International kama Mshauri kuhusu Virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa Kanisa na Wabia wa Asasi za Kidini. Yeye pia ana uambukizo wa Virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Katika mkanda huu, Kasisi Kiongozi Gideon anatushirikisha mambo aliyojifunza katika safari yake ya kuwa na Virusi vinavyosababisha UKIMWI. Anaelezea uzito halisi wa janga la UKIMWI, na anatoa wito wa uhitaji wa kupata ujumbe husika zaidi na sahihi katika kuzuia kuenea kwa Virusi vinavyosababisha UKIMWI. Anawaasa Wakristo waache mitazamo ya kuhukumu watu wenye Virusi vinavyosababisha UKIMWI, na badala yake kuwapa upendo na msaada. Anawatia moyo makanisa kueneza matumaini - sio hofu - kupitia uelimishaji rika, unasihi, huduma majumbani, msaada halisi na maombi.

Naweza Kufanya Nini? (muda: dakika 49 na sekunde 10) umegawanyika katika vipengele vifupivifupi 14 juu ya mada kama vile ‘Kuvumilia unyanyapaa’, ‘Kwanini upinwe uambukizo wa Virusi vinavyosababisha UKIMWI?’ na ‘Changamoto kwa Kanisa’. Mwongozo tofauti wa Mwezeshaji, ukiwa pamoja na maainisho ya utepe wa sauti, pia unapatikana.

FOCAGIFO na Strategies for Hope.

 

2004; dakika 49.

Please tell your friends about this page: